Mfalme Charles na Waziri Mkuu Rishi Sunak waliiongoza Uingereza leo Jumapili katika kuwakumbuka waliokufa katika vita vya nchi hiyo, wakitaka kuiunganisha jamii siku moja baada ya kufanyika maandamano makubwa yanayoiunga mkono Palestina ambapo maandamano hayo yalishuhudia mapigano kati ya waandamano wa mrengo wa kulia na polisi.
Katika sherehe ya kumbukumbu ya vita ya Cenotaph huko Whitehall katikati mwa London, Charles, Sunak, wakiwa na wanasiasa wengine na wanachama waandamizi wa familia ya kifalme walikaa kimya kwa dakika mbili na kisha kuweka mashada ya maua kuwaenzi wale waliouawa katika vita.
Siku ya Jumamosi, maadhimisho ya kila mwaka ya Armistice Day, ya kumalizika kwa Vita vya Dunia yalishuhudia zaidi ya waandamanaji 300,000 wanaoiunga mkono Palestina wakiandamana katikati mwa London, huku polisi wakiwakamata zaidi ya watu 120 katika juhudi za kuwazuia waandamanaji wa mrengo wa kulia kuvamia maandamano mengine.