Hali ya mazingira ya afya yanazidi kuzorota nchini Sudan; yanasema mashirika ya UN

Mfano wa hali ya mazingira ya kiafya nchini Sudan

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaonya hali ya afya inazidi kuzorota nchini Sudan na nchi jirani wakati idadi inaongezeka ya ya watu wanaokimbia mapigano kati ya jeshi la Sudan na vikosi vya Rapid Support Forces.

Kabla ya mgogoro huo kuzuka Aprili 15, Wa-sudan milioni 4.5 tayari walikuwa wamekoseshwa makazi yao, zaidi ya watu milioni 3.7 ndani ya Sudan na wengine 800,000 kama wakimbizi nchini Chad, Sudan Kusini, Misri na Ethiopia. Tangu majenerali wanaohasimiana walipoingia katika vita shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) linasema takribani idadi sawa ya watu milioni nne wameachwa bila makaazi.

Hali ndani ya Sudan, ambako timu za UNHCR zipo, haziwezi kukidhi mahitaji ya kibinadamu ambayo yanazidi kuongezeka na hayaendani kutoa rasilimali zilizopo alisema William Spindler, msemaji wa UNHCR.