Kundi linalofuatilia haki za kibinadamu za waarabu siku ya jumatatu lilitoa wito wa msaada wa kimataifa kwa takribani wahamiaji 360 wa kusini mwa jangwa la Sahara ambao maafisa wa Libya wanasema waliokolewa baada ya kutelekezwa katika jangwa na polisi wa Tunisia kwenye mpaka na Libya.
Arab Organisation for Human Rights (AOHR) yenye makao yake Cairo ilisema lilikaribisha mapokezi ya Libya kwa wahamiaji ambao walishuhudia hali ngumu ya kibinadamu kabla hawajachukuliwa na walinzi wa mpakani wa Libya.
“kulingana na walinzi wa mpaka wa Libya, wahamiaji 360 wakiwemo wanawake na watoto wanahitaji msaada wa habara wa kibinadamu na madawa, kiongozi wa AOHR alisema, akiwasihi maafisa wa Libya kuidhinisha wasi wasi huo wa kimamlaka, kamishna wa cheo cha juu katika Umoja wa Mataifa kwa haki za binadamu na taasisi ya kimataifa kwa wahamiaji, kukutana nao na kuwasaidia utaratibu wa kisheria.