Tunisia limekuwa taifa la karibuni la kiarabu kurejesha tena uhusiano wa kidiplomasia na Syria baada ya kuvunjika 2012. Rais wa Tunisia Kais Saied mapema mwezi huu kwamba ameielekeza wizara ya mambo ya nje kuteuwa balozi mpya nchini Syria. Hatua yake imejibiwa na serikali ya Syria kwa kuteua balozi wake wa Tunisia kupitia taarifa ya pamoja kutoka wizara za mambo ya nje za mataifa hayo mawili Jumatano, kulingana na chombo cha habari kinachomilikiwa na Syria cha SANA.
Syria kwa muda mrefu imetengwa na mataifa ya kiarabu kutokana na msako mkali sana uliofanywa na rais Bashar al Assad dhidi ya waandamanaji na kisha dhidi ya raia, suala lililogeuka na kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe kuanzia 2011. Hali hiyo ilipelekea Syria kuondolewa kwenye uanachama wa jumuiya ya mataifa ya kiarabu wakati Tunisia ikifunga ubalozi wake mjini Damascus. Ujumbe wa Syria ukiongozwa na waziri wa mambo ya nje uliwasili Saudi Arabia Jumatano kwa mazungumzo kuhusu uhusiano wa pamoja kati ya mataifa hayo mawili, shirika la habari la Syria liliripoti.
Saudi Arabia ni mwenyeji wa kongamano la mwezi ujao la jumuiya ya mataifa ya kiarabu, ambapo mataifa mengi yana matumaini makubwa kwamba uanachama wa Syria utarejeshwa, amesema katibu mkuu wa jumuiya hiyo Aboul Gheit.