Afisa wa juu wa  Marekani : Wanajeshi wa Eritrea bado wako Ethiopia

Mtu mmoja akivuka karibu na lori lililoharibiwa kwenye barabara inayoelekea mji wa Abi Adi, katika eneo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia wakati wa mapigano Mei 11, 2021.

Afisa wa juu wa  Marekani alisema Jumamosi kwamba wanajeshi wa Eritrea bado wako nchini Ethiopia ingawa wameondoka mpakani, kinyume na mamlaka ya Ethiopia ambayo inasema kuwa Waeritrea tayari wameondoka.

Wanajeshi wa Eritrea walipigana pamoja na wanajeshi wa Ethiopia na wanamgambo washirika katika mzozo wa miaka miwili uliowahusisha serikali ya Ethiopia dhidi ya vikosi vya waasi katika eneo la kaskazini la Tigray.

Mwezi Novemba, hata hivyo, serikali ya Ethiopia na vikosi vya Tigray vilitia saini makubaliano ya kumaliza uhasama. Mkataba huo uliamuru kuondolewa kwa vikosi vyote vya kigeni kutoka Tigray.

“Kuhusiana na Waeritrea tunaelewa kuwa wamerudi mpakani na wametakiwa kuondoka,” Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Linda Thomas-Greenfield, alisema katika mkutano na waandishi wa habari alipoutembelea mji mkuu wa Kenya Nairobi.