Mamlaka Korea Kaskazini imeamuru kufungwa kwa mji wa Pyeongyang

Mji wa Pyeongyang

Ilani ya serikali ya Korea Kaskazini iliyotangaza kufungwa huko haikutaja COVID-19, NK News ilisema. Haijabainika ikiwa ufungaji huo  ulijumuisha maeneo zaidi ya Pyeongyang

Mamlaka ya Korea Kaskazini imeamuru kufungwa kwa siku tano katika mji mkuu wa Pyeongyang huku kukiwa na ongezeko la magonjwa yasiyojulikana ya kupumua, kulingana na wanadiplomasia wa Russia na chombo cha habari chenye makao yake mjini Seoul.

NK News, chapisho lenye vyanzo vya habari nchini Korea Kaskazini, liliripoti kwa mara ya kwanza kufungwa kwa shughuli za umma-LOCKDOWN likisema wakaazi wa Pyeongyang wanatakiwa kubaki majumbani mwao na kufanyiwa uchunguzi wa lazima wa joto la mwili kuanzia Jumatano hadi Jumapili.

Ilani ya serikali ya Korea Kaskazini iliyotangaza kufungwa huko haikutaja COVID-19, NK News ilisema. Haijabainika ikiwa ufungaji huo ulijumuisha maeneo zaidi ya Pyeongyang.

Katika chapisho kwenye Facebook, Ubalozi wa Russia mjini Pyeongyang lilithibitisha "kipindi maalum cha kupambana na janga hilo" kilitangazwa mjini humo kutokana na kuongezeka kwa homa ya msimu hivi karibuni na "magonjwa mengine ya kupumua".