Mmoja wa wataalamu wakuu wa afya nchini China wameonya juu ya kuongezeka kwa visa vya Covid-19, vyombo vya habari vya serikali vimesema Jumapili, kufuatia uamuzi wa serikali wa kuachana na mkakati wake mkali wa virusi vya corona.
Maduka na migahawa mjini Beijing yametelekezwa wakati nchi hiyo ikisubiri ongezeko la maambukizi kufuatia uamuzi wa kupunguza wigo wa upimaji wa lazima, kuruhusu baadhi ya kesi za COVID kujiweka karantini nyumbani pamoja na kusitisha mkakati mkubwa wa kufunga huduma zote za jamii.
Mtaalamu wa magonjwa ya milipuko Zhong Nanshan aliviambia vyombo vya habari vya serikali katika mahojiano yaliyochapishwa Jumapili kwamba virusi vipya aina ya Omicron vilivyoenea nchini China vinabadilika sana na vinaweza kusababisha kuongezeka kwa visa vya maambukizi.
"Mabadiliko ya sasa ya Omicron yanaambukiza sana na mtu mmoja anaweza kusambaza kwa watu 22," alisema Zhong, mshauri mkuu wa serikali katika kipindi chote cha janga hilo.
"Kwa sasa, janga la virusi vya magonjwa ya milipuko nchini China vinasambaa haraka, na kutokana ya hali kama hizo, bila kuzingaria njia mbadala za kuzuia na kudhibiti, itakuwa vigumu kusitisha njia za maambukizi." Kulegezwa kwa sera ya Sera ya China inayoitwa "zero-Covid" ilifuatiwa na maandamano ya nchi nzima yanayopinga sera hiyo ambayo ilikuwa imeathiri uchumi na kuwafungia mamilioni majumbani mwao.