DRC inasema haiwezi kufanya mazungumzo ya amani na M23 ikiwaita ni "magaidi"

Your browser doesn’t support HTML5

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imesema haitafanya mazungumzo na kundi la waasi la M23 ikilitaja kundi hilo ni la kigaidi. Msimamo wa serikali unatofautiana na msimamo wa Umoja wa Afrika unaotaka serikali ya DRC kuzungumza na makundi yanayopigana mashariki mwa Congo.