Zimbabwe na Zambia zajadiliana na mashirika ya fedha ya kimataifa kupunguza madeni yao

Sarafu ya Zimbabwe isiyo na thamani yeyote na dola ya Marekani katika biashara ya mitaani.

Mataifa hayo ya kuisni mwa Afrika yenye madeni makubwa na matatizo ya kuchumi yako kwenye mazungumzo na Benki Kuu ya Dunia na IMF kuweza kupunguza madeni yao kwa kupata mashrati nafuu ya ulipaji.

Waziri wa fedha wa Zimbabwe Mthuli Ncube, amewaambia waandishi habari mjini Washington kwamba, Zimbabwe iko kwenye majadiliano na Benki kuu ya Dunia na Shirika la fedha Duniani juu ya namna ya kupunguza madeni yake na wafadhili wa kimataifa.

Zimbabwe ambayo imekumbwa na ughali wa maisha kupindukia mnamo miaka 15 iliyopita, ina deni la kigeni lenye thamani ya dola bilioni 10, na sehemu kubwa ni kutokana na kuchelewa kulipa madeni ya miaka ya nyuma.

Kutokana na hali hiyo nchi hiyo haijapokea mikopo au msaada kutoka mashirika ya fedha ya kimataifa kwa zaidi ya miaka 20 sasa.

Bw. Ncube anasema hivi sasa serikali ya Harare imeanza mipango ya kutoa hundi kuweza kulipa madeni yake na kutoa hundi ili kulipa fidia wakulima wa kizungu walopokonywa mashamba yao.

Zambia yajadili na wafadhili kurekebisha malipo ya deni

Nae waziri wa fedha wa Zambia Situmbeko Musokotwane anasema nchi yake iko na majadiliano na China na wafadhili wa kimataifa juu ya kurekebisha mipango yake ya malipo ya madeni.

Akizungumza pia na waandishi habari baada ya kumalizika kwa mikutano ya Benki Kuu ya Dunia na IMF mjini Washington Musokotwane anasema kutokana na mgomo wa wafanyakazi wa reli na bandari huko Afrika Kusini ni ishara kwamba kanda yao inahitaji miundo mbinu zaidi ya uchukuzi akiongeza kusema kwamba wafadhili wa kimataifa hawakuzingatia mahitaji umuhimu ya mataifa ya Afrika siku za nyuma kua na miundo mbinu.

Wafanyakazi wa reli na bandari wa Afrika Kusini wa Kampuni ya Transnet waendelea na mgomo mjini Cape Town.

Amesema Zambia imekua nchi ya kwanza kutoweza kulipa madeni yake hapo mwaka 2020 katika enzi ya janga la COVID 19, kwa kuchelewa kukamilisha utaratibu wa kulipa madeni yake.

Zambia iliweza kupata b mkopo wa dola bilioni1.3 kwa kipindi cha miaka mitatu kutoka IMF hapo Septemba.