Moto mkubwa umezuka katika daraja linalounganisha Crimea na Russia

Moto umezuka katika daraja kuu linalounganisha Crimea na Russia

Moto mkubwa uliosababishwa na bomu la kwenye gari umezuka katika daraja kuu linalounganisha Crimea na Russia ambalo ililiteka eneo hilo mwaka 2014 Moscow ilisema Jumamosi bila kuilaumu Ukraine mara moja.

Daraja hilo la barabara na njia ya reli lililojengwa kwa amri ya Rais wa Russia Vladimir Putin na kuzinduliwa mwaka 2018 lilikuwa kiungo muhimu cha usafiri kwa kubeba vifaa vya kijeshi kwa wanajeshi wa Russia wanaopigana nchini Ukraine hasa kusini pamoja na kusafirisha wanajeshi kote.

Katika eneo la Mlango bahari wa Kerch ni kivuko pekee kati ya eneo linalokaliwa la Crimea na Russia.

Msemaji wa Kremlin amesema Putin ameagiza kuundwa kwa tume ya kuchunguza mlipuko huo mashirika ya habari ya Russia yameripoti.