Malkia Elizabeth ameidhinisha uteuzi wa Liz Truss kama Waziri Mkuu wa Uingereza leo jumanne na kupewa jukumu la kuiongoza nchi hiyo kupitia kipindi cha kudorora kwa uchumi na mzozo wa nishati ambao unatishia mustakabali wa mamilioni ya familia na biashara. Truss, ni Waziri Mkuu wa nne kutoka chama cha Conservative katika miaka sita alisafiri kwa ndege hadi nyumbani kwa familia ya kifalme huko Scotland kuelezwa na malkia mwenye umri wa miaka 96 kuunda serikali.
Anachukua nafasi inayoachwa na Boris Johnson ambaye alilazimika kujiuzulu baada ya miaka mitatu ya misukosuko madarakani. Truss atakabiliana na moja ya matatizo ya kiongozi yoyote wa baada ya vita nchini Uingereza huku mfumuko wa bei ukiwa umepanda sana, gharama ya nishati imepanda na benki kuu ya uingereza inaonya kuhusu kipindi kirefu cha kudorora kwa uchumi ifikapo mwisho wa mwaka huu.
Mpango wake wa kufufua uchumi kwa kupunguza kodi wakati pia uwezekano wa kutoa karibu dola bilioni 116 ili kukabiliana na gharama za nishati tayari umetikisa masoko ya fedha na kusababisha wawekezaji kuachana kutumia pauni na bondi za serikali katika wiki za karibuni.
Akizungumza Jumapili Truss alimshukuru Waziri Mkuu anayeondoka madarakani Boris Johnson na kuahidi kukabiliana na tatizo la nishati huku akichaguliwa kuwa kiongozi mpya wa chama jumatatu.
Lakini wote tutafanya kwa pamoja kwa ajili ya nchi yetu. nitahakikisha kwamba tunatumia watu mahiri wote wa chama cha consevativu , wabunge wetu mahiri, madiwani wetu, wabunge wa Scotland, madiwani na wanaharakati na wanachama wetu wote. kote nchini kwetu. Kwa sababu marafiki zangu najua tutawasilisha tutawasilishana sisi tutaleta ushindi mkubwa wa chama cha conservative mwaka 2024, Asante.
Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Boris Johnson aliondoka ofisini kwake mtaa wa Downing kwa mara ya mwisho siku ya Jumanne kabla ya kuelekea Scotland kuwasilisha barua rasmi ya kujiuzulu kwa malkia Elizabeth wa II.
Akizungumza akiwa nje ya ofisi yake ya zamani, Johnson alisema sera zake zimeipa nchi nguvu ya kiuchumi ili kuwasaidia watu kukabiliana na shida ya nishati kabla ya kuondoka. “na pia tunatoa masuluhisho ya muda mfupi na muda mrefu kwa mahitaji yetu ya nishati na sio tu kutumia zaidi Haidrokaboni zetu za ndani lakini tunapanda hadi 2030 hna kufikia gigawati 50 za nishati ya upepo. Hiyo ni nusu ya mahitaji ya umeme nchi hii inahitaji kutoka pwani. Upepo pekee, kinu kipya cha nyuklia kila mwaka na kuangalia nini kinatokea ndiyo katika nchi hii, mabadilikao ambayo yanafanyika, ndiyo maana sekta binafsi ya uwekezaji zinafurika. Sekta binafsi zaidi , mtaji wa uwekezaji mkubwa kuliko china yenyewe. makampuni ya teknolojia ya zaidi ya pauni bilioni moja yanachipuka hapa uingereza kuliko ufaransa , ujerumani na Israel”.