Malalamishi yaibuka Kenya wakati magavana wateule wakijiandaa kuapishwa Alhamisi
Your browser doesn’t support HTML5
Kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Kenya tarehe 9 mwezi Agosti mwaka huu, kwa mujibu wa sheria magavana waliochaguliwa wanatakiwa kuapishwa Alhamisi wiki hii, na matayarisho yanafanyika huku baadhi ya Wakenya wakipinga "kiasi kikubwa cha pesa kinachotumika" kwa hafla hizo kote nchini.