IMF imekubali kufufua mpango wa kuisaidia kufedha Pakistan

Logo ya shirika la fedha la kimataifa (IMF)

Shirika la fedha la kimataifa (IMF) limekubali kufufua mpango wa kuisaidia kifedha Pakistan na kutoa unafuu wakati ambapo bei kubwa ya kimataifa ya uagizaji wa nishati inaisukuma nchi hiyo kwenye uhaba wa pesa huku ikikumbwa na tatizo la malipo.

Taarifa ya IMF ya Jumatano jioni ilisema wafanyakazi wake na maafisa wa Pakistan wamefikia makubaliano kuhusu sera zinazo fanyiwa tathmini za mpango wa ufadhili wa kimataifa wa taasisi ya upanuzi (EFF) kwa Islamabad. Makubaliano yaliyofikiwa na wafanyakazi ikiwa yataidhinishwa na bodi ya IMF yataleta jumla ya malipo chini ya mpango huo hadi karibu dola bilioni 4.2

Waziri wa fedha wa Pakistan, Miftah Ismail alisema katika Twitter kwamba Pakistan hivi karibuni itapokea awamu ya kwanza ya dola bilioni 1.17.

Pakistan iko katika wakati mgumu wa kiuchumi. Mazingira magumu ya nje pamoja na sera za ndani vilichochea mahitaji ya ndani hadi kufikia viwango visivyoweza kudumu, alisema Nathan Porter, ambaye aliongoza timu ya IMF katika wiki za mazungumzo na Islamabad.

Taarifa ya IMF ilibainisha kuwa bodi yake pia itazingatia kurefusha program ya EFF hadi mwisho wa Juni mwaka 2023 na iwapo itaongeza karibu dola bilioni moja. akiba ya fedha za kigeni katika benki kuu imeshuka hadi karibu dola bilioni 9.7 ambazo hazitoshi kugharamia wiki chache za uagizaji bidhaa kutoka nje. Rupia pia ilishuka hadi chini ya historia dhidi ya dola ya Marekani katika wiki za hivi karibuni.