Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ana wakati mgumu kutetea wadhifa wake kisiasa

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson akiwa eneo la ofisini kwake 10 Downing Street mjini London

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson alikuwa akipigania uhai wake wa kisiasa siku ya Jumanne baada ya Waziri wa Fedha Rishi Sunak, na waziri mwingine mwandamizi kujiuzulu ghafla kutokana na kashfa ya hivi karibuni iliyoharibu utawala wake.

Ndani ya muda wa dakika kadhaa kwa kila mmoja Sunak na Waziri wa Afya Sajid Javid walimtumia Johnson barua za kujiuzulu ambazo zililenga uwezo wake wa kusimamia utawala unaofuata viwango.

Akiashiria nia yake ya kubaki madarakani kwa muda mrefu kadri iwezekanavyo Johnson alimteua haraka mfanyabiashara wa zamani Nadhim Zahawi hivi sasa ni Waziri wa Elimu kama waziri wake mpya wa fedha.

Wakati huo huo Steve Barclay aliteuliwa Februari kuweka nidhamu katika utawala wa Johnson alihamishwa kwenda kitengo cha afya. Kujiuzulu kulikuja huku Johnson akiomba radhi kwa kumteua mbunge kuhusika katika kutoa huduma ya uchungaji kwa chama chake hata baada ya kuelezwa kuwa mwanasiasa huyo amekuwa akilalamikiwa kuhusu unyanyasaji wa kingono.