Tunisia imechapisha rasimu ya katiba mpya inayompa Rais mamlaka zaidi

Rais wa Tunisia, Kais Saied

Tunisia siku ya Alhamis ilichapisha rasimu ya katiba mpya inayompa Rais mamlaka makubwa zaidi rasimu hiyo inatazamiwa kupigiwa kura ya maoni Julai 25 mwaka mmoja baada ya Rais Kais Saied kunyakua madaraka makubwa.

Rasimu hiyo mpya ilichapishwa Alhamis jioni katika jarida rasmi chini ya mwezi mmoja kabla ya kura ya maoni. Kama inavyotarajiwa na wengi inapendekeza mfumo kamili wa urais toauti na mfumo wa mseto uliokuwepo wa utawala wa rais na bunge chini ya katiba ya nchi ya mwaka 2014.

Chini ya waraka huo mpya Rais wa Jamhuri hutekeleza majukumu ya kiutendaji akisaidiwa na serikali ambayo mkuu wake atateuliwa na rais na hatokabiliwa na kura ya kukosa imani nae kutoka bungeni.

Rais atakuwa mkuu wa majeshi na atakuwa na jukumu la kutaja au kuteua majaji ambao watapiga marufuku mgomo.