Waandishi wa habari Ethiopia bado wanafanya kazi zao kwa mashaka

Logo ikielezea uhuru wa vyombo vya habari na wanahabari

June 18 ni miezi saba tangu Dessu Dulla alipowekwa jela. Mwandishi wa habari raia wa Ethiopia kutoka Oromia News Network (ONN) anashutumiwa kwa harakati za kuipinga serikali.

Kama atapatikana na hatia anaweza kuhukumiwa kifungo cha maisha jela au hata adhabu ya kifo. Ni mabadiliko ya haraka ya matukio kwa Dessu ambaye alirejea nyumbani kutoka uhamishoni ulaya mwaka 2018 akivutiwa na kile kilichoonekana wakati huo kama kipindi cha mageuzi.

Alianza kazi katika ONN ambapo aliongoza kipindi cha kila wiki cha Under The Shadow of Democracy akiangazia vitisho nchini Ethiopia na mkoa wake anakotoka wa Oromia. “Nilidhani ingekuwa enzi nyingine na kwamba demokrasia na uhuru wa kujieleza unaweza kurejeshwa tena” Dessu aliliambia shirika la habari la Reuters kabla ya kukamatwa kwake Novemba mwaka 2021.

Lakini kwa kweli mambo yanaharibika. Waandishi wengi wa habari wameikimbia nchi na wengine wako jela.