Serikali ya Marekani inajaribu kuzuia hatua za kukwepa vikwazo zinazotumiwa na Russia

Rais wa Russia Vladimir Putin

Serikali ya Marekani ilisema Alhamis ilikuwa inajaribu kuzuia hatua za kukwepa vikwazo zinazotumiwa na wasomi wa Russia akiwemo Rais Vladimir Putin ili kujaribu kuficha na kuhamisha pesa pamoja na kutumia mali za kifahari kote ulimwenguni.

Malengo hayo ni pamoja na udalali wa boti, ndege, maafisa wa Russia na wengine walio karibu na Putin. Boti zinazolengwa ni pamoja na Olympia yenye bendera ya Russia, na Olympia yenye bendera ya visiwa vya Cayman, na boti nyingine mbili, Shellest na Nega zote zinazomilikiwa na makampuni ya Russia.

White House ilisema vikwazo hivyo vipya viliwekwa ili kukabiliana na ukwepaji na kuimarisha vikwazo vyetu ili kuimarisha utekelezaji na kuongeza shinikizo kwa Putin na wawezeshaji wake.

Katika taarifa ya kutangaza vikwazo hivy, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alisema Marekani itaendelea kuwaunga mkono watu wa Ukraine huku ikihimiza uwajibikaji kwa Rais Putin na wale wanaowezesha uvamizi wa Russia.