Rais mteule wa Somalia anakaribisha taarifa kwamba kikosi maalum cha operesheni cha Marekani kitakuwa tena nchini Somalia kusaidia katika mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la al-Shabaab.
Hassan Sheikh Mohamud alimshukuru Rais Joe Biden katika ukurasa wa Twitter siku ya Jumanne akiitaja Marekani “mshirika wa kutegemewa katika azma yetu ya kuleta utulivu na mapambano dhidi ya ugaidi”. Vikosi vya Marekani vimekuwa vikifanya kazi kwa miaka mingi na vikosi vya Somalia katika juhudi zao za kuwadhibiti al-Shabaab ilielezewa na maafisa wa jeshi la Marekani na kijasusi kama mshirika tajiri zaidi na mwenye nguvu wa kundi la kigaidi la al-Qaida.
Lakini mwaka 2020 Rais wa zamani Marekani Donald Trump aliamuru kiasi cha wanajeshi 750 wa Marekani nchini Somalia kuondoka badala yake wakiruhusiwa waingie nchini humo mara kwa mara.