Rais wa Marekani Joe Biden alitangaza Jumanne kwamba tukio lililotokea mwishoni mwa wiki la shambulizi la risasi kwa umma katika mji wa Buffalo kwenye jimbo la New York ambapo kijana mzungu aliyekuwa na bunduki alidaiwa kuwaua watu 10 weusi, kwenye duka la vyakula katika kitendo cha ubaguzi wa rangi ambao ni ugaidi wa ndani ya nchi uliochochewa na mzungu mwenye msimamo mkali.
Biden na mke wake Jill Biden walikutana kwa faragha na ndugu wa watu waliouawa na watu wengine watatu ambao walijeruhiwa katika tukio hilo kwenye duka la Tops Friendly Market kabla ya kuzungumza kwa muda mfupi na wamarekani kuhusu kila mmoja wao kwa kuwataja majina akihutubia kupitia njia ya television kutoka jiji la kaskazini-mashariki mwa Marekani.
Rais Biden alilaani shambulizi hilo akisema kuwa “kundi la watu wazungu wabaguzi ni sumu” ambayo haina nafasi nchini Marekani, hata kidogo.