Naibu rais wa Kenya William Ruto amemuomba msamaha rais Uhuru Kenyatta baada ya muda mrefu wa kuonekana wakitofautiana kisiasa.

Your browser doesn’t support HTML5

Viongozi hao wawili tangu kuchaguliwa kwa muhula wa pili mwaka wa 2017 walionekana wazi wazi kutoshirikiana kisiasa, wakati mara kadhaa Ruto akidai kupokonywa madaraka , huku naye Kenyatta akidai kwamba naibu wake ameondokea majukumu yake na kujihusisha kwenye kampeni za mapema.