Wanamgambo wa Libya wanaoungwa mkono na serikali yenye nguvu siku ya Alhamis walikanusha tuhuma za mauaji, mateso, na kazi za kulazimishwa wakisisitiza kuwa wanashikilia sheria na kutishia kuishitaki Amnesty International kwa ripoti yake.
Amnesty siku ya Jumatano iliishutumu The Stability Support Authority (SSA) kwa msururu wa mateso ikiwa ni pamoja na mauaji kinyume cha sheria, kuwaweka watu kizuizini kiholela, kutekwa, na kuzuiliwa kiholela kwa wahamiaji na wakimbizi, kazi za kulazimishwa na ukiukaji mwingine wa kushangaza wa haki za binadamu.
Ilisema inafuata sheria ya Libya na inawawajibisha wanachama wake kwa kitendo chochote kinachofanywa kinyume cha sheria. Kundi hilo pia lilisema linaweka pembeni haki ya kuishtaki Amnesty International kwa kuharibu na kuleta kashfa dhidi ya serikali ya Libya na taasisi zake rasmi.
SSA iliundwa chini ya mamlaka ya Waziri Mkuu wa zamani Fayez al-Sarraj mwezi Januari mwaka 2021 inaongozwa na Abdel Ghani al-Kikli mmoja wa wanaume wenye ushawishi mkubwa zaidi katika mji mkuu wa Tripoli kwenye nchi hiyo iliyopo Afrika kaskazini.