Waandishi wa habari katika nchi zote mbili za Sudan na Sudan Kusini wanasema vitisho, ukandamizwaji, na ukamataji holela ni sehemu ya maisha ya kila siku, na hivyo kupunguza uwezo wao wa kuupa habari umma.
Sudan Kusini inashika nafasi ya 128, na Sudan inashika nafasi ya 151 kati ya nchi 180 katika orodha ya kila mwaka ya uhuru wa vyombo vya habari duniani iliyotolewa Jumanne na Reporters Without Borders ikiendana na utambuzi wa kila mwaka wa Umoja wa Mataifa wa siku ya uhuru wa habari duniani.
Kadri idadi inavyokuwa kubwa, ndivyo hali ya vyombo vya habari inavyozidi kuwa mbaya zaidi. Irene Ayaa wa Association for Media Development in South Sudan anasema udhibiti wa serikali katika nchi yake umeshamiri. Mwezi uliopita tulisajili nakala nne zilizoondolewa kutoka kwenye magazeti, alisema.
Kati ya Januari na mwezi Machi pekee, maafisa wa usalama waliondoa makala kadhaa kutoka kwa gazeti la Juba Monitor, Anna Namiriano ambaye ni mhariri wa gazeti la kila siku la lugha ya kiingereza alikiambia kipindi cha South Sudan in Focus cha VOA. Waliondoa taarifa na tuliacha nafasi hiyo wazi. Wanasdema kwa nini hatuwasikilizi kwa hivyo basi Machi 17 walisitisha gazeti hilo.