Watu 16 wamefikishwa mahakamani kwa kuwauzia silaha wanamgambo huko DRC

Ramani inayoonyesha eneo la North Kivu na Ituri nchini DRC

Watu 16 wakiwemo wanajeshi tisa walifikishwa mahakamani siku ya Jumatatu nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wakituhumiwa kuuza silaha kwa kundi la wanamgambo huko kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo. Silaha za jeshi zinashukiwa kuangukia kwenye mikono ya kundi lenye sifa mbaya la CODECO linalolaumiwa kwa mauaji ya kikabila katika jimbo la kaskazini-mashariki la Ituri.

Silaha hizo zinadaiwa zilitumika katika mashambulizi kwenye vijiji na kambi za watu wasiokuwa na makazi.

Katika shambulizi moja, zaidi ya watu 60 huko Plaine Savo kwenye eneo la Djubu waliuawa hapo Februari mosi mwendesha mashtaka wa kijeshi Joseph Makelele aliiambia mahakama.

Siku ya kwanza ya kesi katika mahakama ya kijeshi huko Ituri iliwatambua washtakiwa na silaha zilizonaswa ambazo ni bunduki aina ya AK47 na mamia ya risasi.

Wanajeshi tisa walioshtakiwa ni pamoja na lutein kanali na mameja watatu.

Washtakiwa hao wa kiraiaa ni pamoja na wanawake wane, mmoja wao alikamatwa mwezi uliopita akiwa na risasi ambazo inasemekana alikuwa akizipeleka kwa wanamgambo wa CODECO katika mkoa wa Kobu.

Pamoja na mauzo haramu ya silaha, washtakiwa hao pia wanashtakiwa kwa uhalivu wa vita, kushiriki katika harakati za uasi na kushirikiana na wahalifu.

CODECO kirefu chake ni Cooperative for the Development of the Congo ni kundi la kisiasa na kidini ambalo linadai linawakilisha maslahi ya kabila la walendu.

Jamii za walendu na wahema zina mzozo, zina mzozo wa muda mrefu ambao ulisababishwa vifo vya maelfu ya watu mwaka 1999 na mwaka 2003 kabla ya uingiliaji kati wa kikosi cha kulinda amani cha ulaya.