Korea Kusini na Marekani wanajiandaa kwa uwezekano wa jaribio la kombora

Watu wakiangalia kwenye TV mfano wa jaribio la nyuklia la Korea Kaskazini. Jan. 25, 2022.

Korea kusini na Marekani wanajiandaa kwa uwezekano wa jaribio la nyuklia la Korea kaskazini huku mivutano ikiwa juu baada ya onyo la wiki hii kutoka Pyongyang, kwamba iko tayari kutumia silaha za nyuklia dhidi ya jirani yake wa Kusini. Jaribio la nyuklia litakuwa la kwanza kwa Korea kaskazini tangu mwaka 2017.

Wataalamu wanasema kwamba pamoja na matamshi ya hivi karibuni ya kivita kutoka Kaskazini, huwenda ikaushinikiza utawala wa Biden na serikali ya Rais ajaye Korea kusini, Yoon Suk-yeol kuchukua msimamo mkali zaidi kuhusu Pyongyang.

Kim Yo Jong, dadake kiongozi wa Korea kaskazini, Kim Jong Un, na makamu mkurugenzi wa idara ya kamati kuu ya chama cha wafanyakazi cha Korea, alizidisha mivutano kwa matamshi yaliyoripotiwa na wengi siku ya Jumanne.

Iwapo Korea kusini itachagua mapambano ya kijeshi na sisi, kikosi chetu cha kupambana na nyuklia kitalazimika kutekeleza wajibu wake bila shaka, alisema. Kim Yo Jong anahudumu kama msemaji wa Korea kaskazini dhidi ya Korea kusini na Marekani.