Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson kama ilivyotarajiwa alitangaza Jumatatu kumalizika kwa masharti yote ya ndani ya COVID-19 kuanzia Novemba 24 hata kujitenga kwa wale waliopimwa na kukutwa na maambukizi.
Akizungumza mbele ya bunge Johnson alisema taifa bado litawahimiza wale wanaopima virusi au wanaopata dalili za virusi hivyo kukaa nyumbani, angalau hadi April mosi wakati serikali itawahimiza watu waliokutwa na maambukizi au dalili kujikinga kibinafsi.
Katika hilo serikali pia itaacha kulipia upimaji wa COVID-19. Johnson alitangaza kuondolewa kwa masharti hayo huku akimtakia kila la kheri, Malkia Elizabeth baada ya kupimwa na kukutwa na COVID-19 siku ya Jumapili. Waziri Mkuu alisema majibu ya malkia juu ya kirusi hicho ni ukumbusho kwamba janga hili bado halijaisha.
Wanasayansi pamoja na wanasiasa wengine wa upinzani wanaonya kwamba kusitisha upimaji na ufuatiliaji wote wa COVID kutadhoofisha uwezo wa kufuatilia ugonjwa huo na kujibu maambukizi yeyote mapya.