Pheneas Munyarugarama anatafutwa kwa kushiriki mauaji ya halaiki Rwanda.

Mafuvu ya waathirika wa mayazi ya malaika ya Rwanda yamehifadhiwa ndani ya kanisa katoliki huko Ntarama, Rwanda, April 5, 2019.

Pheneas Munyarugarama Kanali wa zamani wa Luteni katika jeshi la Rwanda, anatafutwa kwa kushiriki katika mauaji ya halaiki ya 1994 nchini Rwanda.

Munyarugarama anatuhumiwa kuandaa na kushiriki katika mauaji na ubakaji wa Watutsi mnamo Aprili 1994 na kwa kuagiza wale walio chini ya amri yake, wakiwemo raia, na wanamgambo wa Interahamwe kushiriki.

Chini ya amri yake, askari kutoka kambi ya jeshi la Gako walidai kuwauwa raia wapatao 800 kati ya Aprili 7 na Aprili 15, 1994.

Kwa uhalifu huu na shutuma nyingine Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Rwanda, ilimshtumu Munyarugarama kwa tuhuma za mauaji ya halaiki, uhalifu dhidi ya ubinadamu, na uhalifu wa kivita na ilitoa hati ya kukamatwa kwake.

Marekani inashirikiana na serikali zingine, Umoja wa Mataifa na Mahakama ya kimataifa ya mauaji ya Rwanda kufanya iwe vigumu kwa Munyarugarama na wengine wanaohusika na mauaji ya halaiki ya Rwanda kuendelea kukimbia haki. Ili kufanikisha haya mwisho huo, Marekani inatoa malipo ya kufikia hadi dola milioni 5 kwa habari itakayopelekea kukamatwa kwake.

Ikiwa wewe au mtu yeyote unayemjua ana habari juu ya shughuli za Pheneas Munyarugarama na wapi alipo unaweza kuifikisha kwa usiri kamili. Tafadhali tembelea ubalozi ulio karibu nawe wa Marekani au tovuti ya ubalozi ili uwasiliane na Ofisi ya Usalama ya kanda, tuma barua pepe kwa Mpango wa zawadi wa Marekani dhidi ya Vita vya Uhalifu WCRP@state.gov, au wasiliana nasi kupitia WhatsApp kwa nambari + 1-202-975-5468.

Unaweza pia kutembelea ukurasa wetu wa Facebook kwa www.facebook.com/warcrimesrewardsprogram au fuatana nasi kwenye Twitter kwa www.twitter.com/WarCrimesReward kwa picha za hao wanaotafutwa.