DRC yawataka wananchi wachukuwe tahadhari baada ya mgonjwa wa kwanza kuripotiwa

Dkt. Eteni Longondo, Waziri wa afya wa DRC akizungumza na waandishi habari mjini Kinshasa, 10 marchi 2020. (VOA/Lingala)

Waziri wa afya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Eteni Longondo ametoa wito kwa watu kua utulivu na kuzingatia usafi kwa kuosha mikono yao mara kwa mara.

Akizungumza nawaandishi habari mjini Kinshasa siku ya Jumanne, Dkt Longondo amethiubitisha kwamba mtu wa kwanza kuambukizwa na virus Corona anatibiwa mashariki maw mji wa Kinshasa.

Mgonjwa huyo ni Mkongo wa miaka 52 anaishi Ufaransa, ambaye aliingia nchini humo siku ya Jumapili na alikuwa amewekwa karantini baada ya uchunguzi aliofanywa katika uwanja wa ndege wa Kinshasa kubaini kuwa ana ishara za mtu aliyeambukizwa na virusi hivyo.

Waziri wa aya anasema hivi sasa serikali inawatafuta watu wote walosafiri pamoja na mgonjwa ili wapimwe na wawekwe karantini pindi watagunduliwa wameambukizwa na virus hivyo.

Kongo ni nchi ya 11 ya Afrika kuthibitisha kwamba kuna wagonjwa waloambukizwa na virusi vya Covid-19 nchini mwao.

Dkt Longondo amesisitiza kwamba srikali inaimarisha juhudi za uchunguzi katika viwanja vyake vinne vikuu vya ndege kwa kuwakagua kwa makini wasafiri walio na viwango vya juu vya joto, hatua ambayo imekuwa ikichukuliwa kama sehemu ya kupambana na maaambukizi ya virusi hatari vya Ebola.