Bondia Hassan Mwakinyo awashangaza wengi

Your browser doesn’t support HTML5

Mahojiano na mwakilishi wa bondia Juma ndambile

Bondia wa Tanzania, Hassan Mwakinyo amewashangaza wengi baada ya kupata ushindi dhidi ya Mwingereza Sam Eggington lililofanyika Birmingham, Uingereza, Jumamosi.

Mwakinyo mwenye umri wa miaka 23 na ambaye anapigana katika uzito wa super welterweight alishinda katika raundi ya pili kwenye pambano ambalo lilipangwa kwenda raundi 10.

Alishiriki katika pambano hilo kama bondia mbadala baada ya kupewa taarifa ya wiki mbili tu, lakini timu yake inasema Mwakinyo ni bondia ambaye ana bidii sana kwenye mazoezi na kwamba wakati wote yupo tayari.

VOA Swahili ilizungumza na mwakilishi wa bondia huyo, Juma Ndambile, na kwanza kumtaka aeleze Hassan Mwakinyo ni nani?