Ulinzi mkali umeimarishwa katika uwanja wa Luzhniki, mjini Moscow nchini Russia ambapo kutafanyika ufunguzi wa Kombe la Dunia Russia 2018 muda mchache ujao.
Mashabiki tayari wameshajisogeza uwanjani hapo kushihudia ghafla ya ufunguzi itakayofuatiwa na mchezo baina ya wenyeji Russia na Saudi Arabia.
Your browser doesn’t support HTML5
Russia imepeleka maelfu ya polisi katika miji yote 11 itakayokuwa mwenyueji wa mashindano hayo yatakayo chukuwa mwezi mmoja.
Serekali ya Russia ipo makini kutokana na kumbukumbu ya tukio la kigaidi lililofanyika mjini Marseille nchini Ufaransa mwaka 2016, katika mchezo wa mashindano ya Ulaya.