Trump aridhika na mazungumzo pamoja na Kim

Trump na Kim wapeana mkono baada ya kutia saini taarifa baada ya mkutano wao.

Rais Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un wamemaliza mazungumzo ya kwanza ya kihistoria kwa kutia saini taarifa juu ya ahadi za kuangamiza silaha za nuklia za Korea Kaskaizni.

Trump akizungumza baada ya kutia saini hati hiyo amesema ameridhika kabisa na mazungumzo na wameanzisha uhusiano mzuri kati yao.

"Ninadhani uhusiano kamili kati yetu na Korea Kaskazini utabadilika na kua tofauti na namna ilivyo kua awali na tumeweza kukuza uhusiano mzuri kuliko vile tulivyotarajia."

Akiulizwa ikiwa atamalika Kim Washington alijibu, Bila shaka.

Kim kwa upande wake amesema wamekubaliana kuacha nyuma yaliyopita na kufungua ukurasa mpya wa uhusiano.

Kabla ya kutia saini Trump na Kim walikutana kwa mara ya kwanza na kupeana mkono asubuhi katika hoteli ya Capella kwenye kisiwa cha mapumziko cha Sentosa, huko Singapore.

Hapo tena wakakutana ana kwa ana kwa karibu dakika 40, kabla ya kutoka na kukutana pamoja na wajumbe wao wa vyeo vya juu. Katika mkutano huo kulikuwepo mawaziri wa mambo ya nchi za nje na wakuu wa usalama wa taifa wa kila upande.

Walipomaliza mazungumzo hayo viongozi hao walikula chakula cha mchana wakiendelea na mazungumzo bila yakufahamika kile walichokua wanazungumza.

Miongoni mwa masuali muhimu ni namna ya kuangamiza kabisa silaha za nuklia za Korea kaskazini, kuondolewa kwa wanajeshi wa Marekani huko Korea Kusini, suala la wajapan walotekwa nyara, kuheshimiwa haki za binadam

Korea Kaskazini, kuondolewa vikwazo na ushirikiano wa baadae kati ya nchi hizi mbili.

Waziri wa ,mambo ya nchi za nje wa Marekani Mike Pompeo mapema alisema vikwazo havitaondolewa hadi pale mpango wote wa nuklia umeharibiwa