Trump akutana na Kim kwa mkutano wa kihistoria Singapore

Rais wa Marekani Donald Trump akipeana mkono kwa mara ya kwanza na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, katika hoteli ya Capella kwenye kiswa cha Sentosa, Singapore.

Rais Donald Trump wa Marekani na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un wamaliza mkutano wa pili wakati wa chakula cha mchana katika ukumbi wa mkutano wa Sentosa, Singapore siku ya Jumanne June 12, 2018.

Miongoni mwa maafisa wakuu wanaoshiriki kwenye mikutano hiyo ni waziri wamambo ya nchi za nje Mike Pompeo, mkuu wa utawala wa White House John Kelly na mshauri wa usalama wa Taifa John Bolton upande wa Marekani. Kwa upande wa Korea Kaskazini yupo Kim Yong Chol, mshauri wa juu wa Kim aliyetembelea Washington hivi karibuni na Waziri wa mambo ya nchi za nje.

Mapema baada ya kukutana kwa mara ya kwanza Trump alisema mkutano wake na Kim ulikua "mzuri mzuri sana" na kusema watakua na "uhuisnano mzuri kabisa", alipozungumza kwa ufupi na waandishi habari.

Awali viongozi hao wawili walikutana kwa dakika 40 ana kwa ana wakiwa na wakalimani wao pekee yao. Hapo tena wakakutana pamoja na wajumbe wao kwa saa moja nyingine.