Obama asema maadili yakikiukwa hatonyamaza kimya

Rais wa Marekani Barack Obama akijibu swali la waandishi wa habari katika mkutano wa APEC

Rais barack Obama alipokutana na viongozi wa mataifa 21 Asia na Pacific –APEC, bado amesisitiza uungwaji mkono wake katika ushirikiano wa kimataifa wa biashara na alikubali kuwa maamuzi hayapo kwake tena.

Rais wa Marekani Barack Obama amemaliza ziara yake ya masuala ya kigeni huko Peru kama jinsi alivyoanza katika bara Ulaya, akijaribu kuwahakikishia viongozi wa dunia ambao wanahofu kuhusu mabadiliko ya utawala wa Marekani wakizingatia zaidi sera za kigeni za Marekani chini ya rais mteule Donald Trump.

Rais barack Obama alipokutana na viongozi wa mataifa 21 Asia na Pacific –APEC, bado amesisitiza uungwaji mkono wake katika ushirikiano wa kimataifa wa biashara na alikubali kuwa maamuzi hayapo kwake tena.

Viongozi wa dunia wakiwa kwenye mkutano wa Apec

Mwishoni katika mkutano na waandishi wa habari Obama alitoa maneno magumu ya ushauri kwa kiongozi ajaye Marekani akisema kuwa Marekani iko imara katika kulinda sheria za dunia na kuhakikisha amani na uthabiti.

“ kama hatuko upande wa kile kilicho sahihi, kama hajufanyi mjadala na kuusimamia vyema, hata wakati mwingine hatuwezi kushiriki kwa asilimia 100 , utavunjika na hakuna yoyote atakayeweza kuziba uharibifu” alisema rais Obama.

Alipoulizwa kama atashindwa kumkosoa Trump atakapoingia madarakani, Obma alisema ana mpango wa kwenda mapumzikoni na mkewe Michelle na kumpa nafasi rais mteule, lakini amesema anaweza kuzungumza kama ataona maadili yanakiukwa.