Kesi ya kupinga ushindi wa rais Museveni wa Uganda katika uchaguzi mkuu wa Uganda uliofanyika mwezi Februari, imeanza kusikilizwa Jumatatu katika mahakama kuu nchini humo.
Your browser doesn’t support HTML5
mawakili wake aliyekuwa mgombea wa urais Amama Mbabazi walifanyia mabadiliko ya orodha ya mambo mahakama hiyo inafaa kushughulikia, wakitaka hesabu ya kura katika wilaya 42 kurudiwa, jambo ambalo mawakili wa rais Museveni na wale wa tume ya uchaguzi walipinga.
Vikao vya mahakama viliahirishwa mara kadhaa, lakini hatimaye jopo la majaji tisa, wakakubali ombi la Amama Mbabazi.