Wapenda mageuzi huko Iran wanaonekana wanapata ushindi katika uchaguzi wa bunge ulofanyika ijumaa, kutokana na ishara za matokeo ya awali yaliyotolewa Jumapili.
Wapenda mageuzi hao ambao wangelipendelea kuwa na ushirikiano zaidi na nchi za magharibi wamenyakua viti vyote 30 vya jimbo la Teheran.
Your browser doesn’t support HTML5
Rais Hassan Rouhani na rais wa zamani Akbar Hashemi Rafsanjani wanaongoza pia katika uchaguzi wa wajumbe wa baraza la waatalamu, chombo chenye ushawishi mkubwa kinachofuatilia kazi za kiongozi mkuu wa kidini Ayatollah Ali Khameni, ambae ana kauli ya mwisho juu ya sera za kigeni za Iran na anaweza kumteuwa kiongozi ajae wa kidini.
Your browser doesn’t support HTML5
Matokeo ya awali yanaonesha wagombea wa kihafidhina wakipoteza viti katika bunge la taifa lenye viti 290. Mwandishi habari wa Redio Iran Salim Saleh anasema matokeo ya safari hii yanaweza kuleta mabadiliko ya kweli ya kidemokrasia nchini humo.