Museveni apongeza matokeo ya uchaguzi, Besigye anayapinga

Jeshi la Uganda la wekwa katika njia za Kampala baada ya uchaguzi

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametetea matokeo ya uchaguzi wa rais ulofanyika siku ya Alhamis,i akipinga malalamiko ya upinzani kwamba kulikua na wizi wa kura.

Your browser doesn’t support HTML5

Sunday Shomari na Kennes Bwire waripoti kutoka Kampala

Akizungumza siku ya Jumapili kiongozi huyo wa muda mrefu alisema yeyote anaedai kulikua na wizi wa kura "amepotea akili" akidai hata yeye aliibiwa kura kwani alitarajia kupata zaidi ya asili mia 60 alizopata.

Dr. Kizza Besigye akizungumza na waandishi habari

Akizungumza na Sauti ya Amerika kwa upande wake, kiongozi wa upinzani Dk. Kizza Besigye anasema wanapinga matokeo kutokana na jinsi uchaguzi ulivyofanyika na matokeo yaliyokua yanatolewa na vituo vya kura yalitofautiana na yale yaliyotolewa na tume ya uchaguzi.

Your browser doesn’t support HTML5

Mahojiano na Kizza Besigye

Dk. Besigye akizungumza akiwa amezuliwa nyumbani kwake anasema hawajaamua ni hatua gani watakayochukua, lakini amewataka wafuasi wao wajitayarishe kukaidi amri ya utawala ili kutetea haki zao.