Mkataba wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa Waidhinishwa Paris

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ufaransa Laurent Fabius, (kati), rais mteule wa COP21, na Christiana Figueres, kushoto, katibu mtendaji wa Umoja wa mataifa kwaajili ya mabadiliko ya hali ya hewa wakifurahia huko Le Bourget, France, Dec. 12, 2015.

Wajumbe kutoka zaidi ya mataifa 190 walokutana mjini Paris wameidhinisha mkataba wenye lengo la kupunguza kasi za kuongezeka kwa hali ya joto duniani siku ya Jumamopsi mchana.

Mkataba huo kwa mara ya kwanza unazitaka mataifa yote ya dunia kupunguza uchafuzi wao wa hewa kwa gesi za sumu za greenhouse.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ufaransa, Laurent Fabius aliyeongoza mazungumzo hayo ya wiki mbili, alitaja hati hiyo yenye ukurasa 31 kuwa ni ya kihistoria na kuzitaka nchi za dunia kutia saini mswada wa mkataba huo wenye mipango ya matarajio makubwa.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ban Ki Moon amesema, " Mwisho wa njia umeanza kuonekana. Hebu tukamilishe hii kazi."

Rais Barack Obama wa Marekani amesema mkutano huo ni kituo cha kubadili ukurasa katika juhudi za kupunguza uchafuzi wa gesi chafu na kupunguza joto duniani.