Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, amesema kuna uwezekano mkubwa na si vinginevyo ndege ya abiria ya Russia ililipuliwa kwa bomu katika Penysula ya Sinai nchini Misri wiki iliyopita na kuuwa watu wote 224.
Akiongea na Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sissi mjini London, Alhamisi, Bwana Cameron pia amegusia kwamba wataalamu bado hawajajua chanzo halisi cha ajali hiyo.
Afisa mmoja wa Marekani amesema mawasiliano yaliyoingiliwa inawezekana kwamba Islamic State walihusika kuiangusha ndege hiyo.
Vilevile amedai mtu mmoja ndani ya uwanja wa ndege wa Sharm el-Sheikh alisaidia kutega bomu katika ndege ya shirika la Metrojet A-321 iliyokuwa ikielekea St. Petersburg.
Lakini maafisa wa Misri na Russia wanakataa kwamba kuna ushahidi wowote utaoweza kuthibitisha hilo.
Msemaji wa ikulu ya Russia, Kremlin, Dmitry Peskov, amesema kwamba kujumuisha chochote kila kabla ya uchunguzi inabaki kuwa ni tetesi.
Naye msemaji wa rais wa Misri ametahadharisha kuhusu kuamini suala hilo kwa sasa.