Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania na mbunge wa Jimbo la Handeni Tanga Mhe.Abdalah Kigoda amefariki dunia jana Oktoba 12, 2015, nchini India alikokuwa anapata matibabu, ambayo haikuelezwa rasmi.
Ofisi ya bunge la Tanzania imethibitisha habari za kifo hicho na taarifa zaidi kuhusu taratibu za kusafirisha mwili wa marehenmu na mipango yote ya mazishi zitatolewa na serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na familia ya marehemu na ofisi ya bunge nchini humo.
Dr.Kigoda alizaliwa mwaka 1953 na kupata shahada yake ya kwanza katika chuo kikuu cha Daresalaam , shahada ya uzamili katika chuo kikuu cha Vanderbilt hapa Marekani na Phd katika chuo kikuu ch Missouri katika masuala ya uchumi.
Alishikilia nyadhifa ya wizara mbali mbali kuanzia 1995 hadi kua waziri wa viwanda na biashara katika serikali ya pili ya Rais Jakaya Kikwete.