Watu zaidi ya 700 wafariki katika mkanyagano Mecca

Wafanyak\azi wa huduma za dharura wakihudumia waathirika wa mkanyagano.Septemba 24, 2015.

Watu wasioungua 717 wamefariki dunia na wengine 805 kujeruhiwa baada ya mkanyagano katika hijja ya kila mwaka ya waislam nje kidogo ya mji wa Mecca.

Maafisa wa Saudia Arabia wanasema tukio lilitokea alhamisi huko Mina ambako mahujaji wanarusha mawe kwenye minara inayowakilisha shetani katika hatua ya mwisho ya hijja kabla ya kuanza kwa sherehe za Eid al HAJJ.

Idara ya kulinda raia ya Saudia Arabia ilitoa idadi ya waathirika katika akaunti yake ya Twitter na kutoa picha zikionyesha wafanyakazi wa huduma ya kwanza wakibeba watu katika machela ikiwa ni pamoja na mmoja akifanyiwa huduma maalum ya moyo.