UKAWA yazindua kampeni ya uchaguzi Tanzania

Mkutano wa UKAWA Jangwani kuzindua kampeni yake 2015

Mkutano wa UKAWA Jangwani kuzindua kampeni yake 2015

Mungano wa vyama vya upinzani Tanzania unaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA, umezidua rasmi kampeni yake ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015, kwa mkutano mkubwa wa hadhara huko Dar Es Salaam.

Wachambuzi wa kisiasa na waandishi habari wanasema mkutano huo ulihudhuriwa na wafuasi wengi kuwahi kutokea kwa tukio la kisiasa tangu kuanza mfumo wa kidemokrasia nchini humo mwaka 1995.

Mgombea rais anaepeperusha bendera ya chama cha CHADEMA, kwa tiketi ya UKAWA, waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa alitangaza vipau mbele vyake akiwa rais.

Your browser doesn’t support HTML5

Jamila Omar azungumzia mkutano wa UKAWA

Amesisitiza kwamba kipau mbele cha kwanza ni elimu, akisema akichaguliwa rais ataidhinisha elimu ya bure kuanzia shule ya msingi hadi vyuo vikuu.

Bw Lowassa, amesema masuala mengine muhimu kwake yeye ni kuimarisha afya, hasa afya kwa kina mama na watoto, miundo mbinu, kilimo cha kisasa na usafiri hasa usafiri wa reli na ndege.

Mwanmdishi wa kituo cha televisheni cha Tanzania cha Chanel 10, Jamila Omar alikua kwenye mkutano huo na anasema cha muhimu ni kwamba mikutano umefanyika kwa amani na mgombea kiti cha rais kusisitiza kwamba mikutano yao ya kampeni itafanyika kwa Amani na kuheshimu sharia.

Viongozi wengine wa upinzani walizungumzia juu ya kunyanaswa kwa vyama vao na wafuasi wao kinyume na misingi ya kidemokrasia.