Waandamanaji wapinga mkutano wa Viongozi wa G7 Ujerumani

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, kushoto, na Rais wa Marekani Barack Obama wanakaribishwa na weakazi wa kijiji cha Kruen, kusini mwa Ujerumani June 7, 2015.

Viongozi wa mataifa saba tajri duniani wanakutana Ujerumani Jumapili, katika mji wa mapumziko wa Garmisch Partenkirchen, kwa mkutano wa kila mwaka wa siku mbili, kujadili mizozo mbali mbali ya kimataifa, pamoja na masuala ya uchumi, mabadiliko ya hali ya hewa, na vita dhidi ya ISIS.

Rais Barack Obama akifuatana na mwenyeji wake Kansela Angela Merkel walitembelea kijiji kimoja karibu na eneo la mkutano Jumapili asubuhi, na kusema kwamba mnamo siku mbili watajadili kile alichokieleza ni "changamoto ngumu", zinazokabili dunia.

Amesema, "tutajadili mustakbal wetu wa pamoja, uchumi wa kimataifa ambao utabuni nafasi za ajira, kuhakikisha Umoja wa Ulaya unaendelea kuwa na nguvu na ufanisi, kubuni ushirika mpya wa biashara kati ya mataifa ya Ulaya na Amerika, na kukabiliana na uvamizi wa Rashia huko Ukraine, pamoja na kupambana na kitisho kutokana na mabadiliko makubwa ya hali ya hewa."

Viongozi hao wanatarajiwa kukubaliana juu ya kuendelea na vikwazo dhidi ya rashia, ambayo ilikuwa mwanachama wa kundi hilo hadi pale ilipoivamia na kukalia jimbo la Crimea, mashariki ya Ukriane mwaka jana.

.