Matokeo ya kihistoria katika uchaguzi mkuu Uingereza

David Cameron pamoja na mkewe Samantha wanawasili kupiga kura katika kituo cha Spelsbury, Uingereza May 7, 2015.

Waingereza wameamka wakipigwa na mshangao kuona jinsi matokeo ya uchaguzi mkuu wa bunge umekuwa tofauti kabisa na uchunguzi mbali mbali wa maoni ulofanywa kabla ya uchaguzi.

Kabla ya Waingereza kwenda kupiga kura Alhamisi uchunguzi ulieleza hakuna chama kitaweza kupata ushindi na huwenda chama cha upinzani cha Labour kitaweza kupata ushindi.

Lakini wakati matokeo yanapotangazwa usiku mzima, Mungano wa vyombo vya habari vya Uingereza unatabiri kwamba chama tawala cha Waziri Mkuu David Cameron cha Conservative, huwenda kikapata ushindi mkubwa na kutokuwa tena na haja ya kuunda serikali ya mungano.

Chama cha upinzani cha Labor kimepigwa na sunami na chama kidogo cha kizalendo cha Scotland cha SNP, ambacho kimeweka historia kwa kunyakua zaidi ya viti 50 kutoka 6 kilivyokua navyo wakati wa uchaguzi wa mwisho.