Ajali barabarani zasababisha vifo zaidi Tanzania.

Ajali Moro.

Wakati serikali ya Tanzania ikiwa imemaliza mgomo wa madereva mwishoni mwa wiki waliogoma kushinikiza matakwa yao ikiwemo kukataa kurudi kwenye vyuo vya usafirishaji , ajali za barabarani nchini humo zimeendela kugharimu maisha ya watanzania walio wengi.

Jumapili ajali nyingine ya barabarani iliyotokea Eneo la Ruaha Mbuyuni kwenye barabara kuu ya Iringa - Morogoro, imepoteza maisha ya watu 19 na wengine kumi na watatu kujeruhiwa vibaya katika ajali hiyo ambapo magari hayo yaliwaka moto na kuteketeza abiria kiasi cha kutotambulika.

Taarifa zilizopatikana Jumatatu zimeeleza kuwa ni miili minne tu iliyotambuliwa na kuzikwa huku miili mingine 15 ikizikwa Jumatatu katika kaburi la pamoja.

Sauti ya Amerika imezungumza na baadhi ya wadau wa usafirishaji jijini Dar es salam kuhusiana na mfululizo huo wa ajali za barabarani nchini, huku wengine wakitupia lawama madereva kwa uzembe na wengine wakizungumzia ubovu wa miundo mbinu.

Ramadhan Kaswelo ni wakala wa usafirishaji katika kituo kikuu cha mabasi ubungo anasema "hakuna kitu kikubwa kinachoathiri madereva kama miundo mbinu ya bara bara hususan kwenye sehemu zenye kona , kuna bara bara nyingine unakuta kwamba barabara kubwa inayopiotwa mpaka na viongozi lakini unakuta ina mashimo ya ajabu, kwa hiyo pale sasa unaweza ukasema kwamba unamshutumu dereva wa lori ambaye amekufa pale pale kwasababu yeye alitoka moja kwa moja akijua anaingai bara barani pasipo kujua kwamba anaweza kuchukua tahadhari gani".

Bwana Kaswelo pia alizungumzia juu ya umuhimu wa kuwepo kwa kozi kwa madereva, jambo ambalo lilisababisha mgomo kwa madereva wa mabasi mwishoni mwa wiki ambapo pamoja na madai ya kutambuliwa ajira zao kwa kupewa mikataba , walipinga agizo la kutakiwa kurudi chuo cha usafirishaji cha taifa, NIT mara wanapoomba upya leseni zao baada ya kuisha muda wa wali

Mgomo wa madereva wa mabasi ya abiria katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania mwishoni mwa wiki ulimalizwa na waziri wa kazi na ajira Gaudensia Kabaka aliyekutana na maderva hao na kukubaliana kuondoa baadhi ya vipengele vilivyowekwa kwa lengo la kudhibiti ajali, kubwa likiwa kutakiwa kufanya mafunzo kila wakati wa kupata leseni mpya na kupewa mikataba na waajiri wao.