Buhari apata ushindi wa uchaguzi wa rais Nigeria

Wafuasi wa mgombea kiti cha rais Muhammadu Buhari na chama chake cha All Progressive Congress (APC) wakisherehekea ushindi wake mjini Kano, March 31, 2015.

Mgombea kiti wa upinzani katika uchaguzi wa rais nchini Nigeria Muhammadu Buhari apata ushindi wa kura milioni mbili laki moja dhidi ya rais Goodluck Jonathan.

Chama cha upoinzani cha All Progrees Congress (APC) kimetangaza kwamba Nigeria inashuhudia historia ikitendeka baada ya kutangaza ushindi katika uchagzui wa rais ulofanyika siku ya Jumamosi.

Msemaji wa APC Lai Mohammed amewambia waandishi habari kwamba"hii ni mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo kwa wapiga kura kuondowa serikali iliyoko madarakani kwa njia ya kidemokrasia."

Aliongeza kusema,"kabla ya hii leo tangu uhuru, ikiwa serikali haipendwi na wananchi huwa inabaki madarakani kwa nguvu au kuondolewa na jeshi."

Tayari mashabiki na wafuasi wa upinzani wameanza sherehe katika ngome za upinzani na mji alikozaliwa Buhari wa Katsina.

Adeale Mutiliba mfanyabiashara anasema, "Jenerali (BUhari) amewahi kuiongoza nchi hii kati ya mwaka 83 na 84 kama kiongozi wa kijeshi, na wakati huo tuna fahamu kile alichokifanya na hivyo tuna matumiani safari hii atafanya mambo mazuri zaidina tunamatumaini makubwa."