Viongozi wa Israel wajadili kuundwa kwa serikali mpya

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu

Rais wa Israel ameanza majadiliano ya siku mbili na viongozi wa vyama vilivyopata viti vya bunge katika uchaguzi mkuu wa wiki ilopita.

Viongozi hao wanahitajika kumpendekeza nani ateuliwe kuwa waziri mkuu mpya atakae unda serikali ijayo.

Viongozi wa vyama sita ambavyo vilipata kura nyingi katika uchaguiz wa jumanne wiki ilopita, walikutana na rais wa Israel Reuven Rivlin.

Bw Rivlin alisema kabla ya mkutano na wajumbe kutoka chama cha Likud kuwa, kwa sababu ya changamoto za kiusalama, kifedha na kijamii zinazowakabili watu wa Israel, angelipendelea kuona serikali ijayo inaundwa haraka iwezekanavyo.

Chama cha Likud kilishinda viti 30 kati ya viti 120 katika bunge la Israel. Na kutokana na hali hiyo, kiongozi wake, waziri mkuu wa sasa Benjamin Netanyahu, huwenda akateuliwa kuunda serikali ijayo ya muungano.

Afisa anaeongoza majadiliano wa chama cha Likud, Ze’ev Elkin, aliomba kuwepo na kipindi kifupi cha mpito.

Rais wa Israel atakutana hii leo na vyamawajumbe wa vyama vilivyobakia na atatanda waziri mkuu mteule baada ya matokoeo rasmi kutangazwa jumatano.