Obasanjo ajiondowa kutoka chama tawala Nigeria cha PDP

Polisi wakilinda usalama wakati waandamanaji mjini Abuja, mji mkuu wa Nigeria wakipinga kuahirishwa kwa uchaguzi mkuu, Feb. 7, 2015.

Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria, akumbwa na pigo kubwa wiki sita kabla ya uchaguzi mkuu kufuatia kujiondowa kwa Rais wa zamnani wa Olusegun Obasanjo kutoka chama tawala cha People’s Democratic, PDP.

Bw Obasanjo mkosaowaji mkubwa wa Jonathan hasa kutokana na namna anavyokabiliana na uwasi wa Boko Haram, na ulaji rushwa, alichana kadi yake ya uwanachama hadharani jana alipokua anazungumza na waandishi habari kutangaza uwamuzi wake mbele ya nyumbani kwake.

Katika taarifa iliyochapishwa na vyombo vya habari nchini Nigeria baba wa demokrasia ya nchi hiyo alisema “hivi sasa mimi ni Mnigeria wa kawaida na niko tayari kufanya kazi na yeyote bila ya kujali chama chake cha kisiasa.”

Bw Obasanjo ni mwanasiasa mashuhuri wa kikanda na kimataifa akiwa mmoja wapo wa waanzilishi wa chama tawala cha PDP, na mlezi wa kisiasa wa Johnathan.

Rais Goodluck Jonathan.

Kiongozi huyo wa zaamani wa kijeshi aliyeleta mabadiliko ya kidemokrasia nchini mwaka kwa kuacha uwongozi wa kijeshi na kugombania kiti cha rais 1999 kuleta utawala wa kiraia, alisema Bila ya Nigeria hapatakuwepo na PDP tena, hivyo kile baadhi yetu tunabidi kutafakarfi ni namna ya kuifanya Nigeria kuwa na nguvu Zaidi.

Msemaji wa PDP Olisa Metuh amesema chama cha pdp kimesikitishwa sana kutokana na kujiondowa kwa chifu Obasanjo katika wakati huu nyeti baada ya kupatiwa jukwa la kuitawala nchi kwa miaka minane.

Gavana wa jimbo la Jigawa mwanachama wa PDP ameiambia Sauti ya Amerika

"Rais Obasanjo ni kiongozi wa nigerioa aliyepigania sana umoja wa taifa hili. Rais Goodluck Jonathan ni kama motto wake , aliyemfikisha madarakani. Kwa hivyo wote wawili ni sawa na baba na mtoto na wote wanawajibu ya kulinda nchi yao."

Katika mahojiano na jarida la Finacial Times wiki iliyopita Bw Obasanjo alimunga mkono mpizani mkuu wa Jonathan, Muhammadu buhari wa chama cha upinzani cha All progressive Congress APC, mtawala wa zamani wa kijeshi mnamo miaka 1980 na kuonekana mtu mwenye msimamo mkali zaidi kuhusiana na usalama na kupambana na rushwa.

Wachambuzi wa kisiasa wanasema kutokana na msimamo huo wa Obasanjon , chama cha PDP kilikuwa kinajitayarisha kumfukuza kutoka chama , lakini kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 77 alisema alipata habari kutoka vyanzo vyake na hviyo kuamua kujiondowa.

Wanajeshi wa NIgeria wapiga doria mjini Abuja

Jeshi la Nigeria kwenye ukurasa wake wa mtandao unamtuhumu Obasanjo kwa kuhusisha masuala muhimu ya usalama wa kitaifa na masula ya kijeshi katika jukwa la kisiasa.

Na tangu tume ya uchaguzi ya Nigeria kuahirisha uchaguzi mkuu kwa wiki sita hadi mwezi ujao kutyokana na kishinikizo cha jeshi wachambuzi na wananchi wamekuwa wakihoji jukumu la vikosi vya usalama katika kutayarisha uchaguzi.