Ufalme wa Saudia wadaiwa kuhusika na shambulizi Marekani.

Mfalme Salman wa Saudia. Riyadh, Jan. 24, 2015.

Mwanachama wa zamani wa mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda aliyesaidia kupanga njama za Septemba 11,2011 Marekani ametoa ushahidi kwamba wafalme wa Saudia Arabia walitoa fedha na misaada mingine kwa kundi hilo la kigaidi.

Zacarias Moussaoui alitoa ushahidi wake kwa mawakili kwa ajili ya waathirika waliouawa wakati ndege zilipogonga jengo la World Trade Center katika jiji la New York na katika majengo ya wizara ya Ulinzi- Pentagon jijini Washington, wakati ndege nyingine ikianguka kwenye uwanja huko Pennsylvania wakati ikiwa njiani kuelekea kwenye jingo lingine la Washington DC.

Moussoui alisema kwamba baadhi ya “maafisa wenye umaarufu sana” wa Saudia walisaidia al-Qaeda ikiwa ni pamoja mwana mgfalme Turki al Faisalambaye zamani alikuwa afisa wa kijasusi wa Saudia Arabia.

Moussaoui pia anasema alikutana ana kwa ana nchini Afghanistan na mwanadiplomasia wa Saudia kutoka ofisi za ubalozi jijini Washington na walizungumza kuhusu njama za kuitungua ndege ya rais wa Marekani Air Force One.

Ubalozi wa Saudia Jumatano, ulisema Moussaoui ni “mhalifu mwenda wazimu” ambaye mawakili wake pia ni “wajinga”

Ubalozi huo ulisema mashambulizi ya Spetemba 11 ni mojawapo ya mashambulizi yaliyopelelezwa sana na hakuna ushahidi unaohusisha maafisa wa Saudia.

Moussaoui alihukumiwa kifungo cha maisha Marekani kwa kushiriki kwake katika mashambulizi hayo ya kigaidi.