Rais Kenyatta apokea ripoti ya kupambana na ugaidi

Ndege ya jeshi la Kenya inayosafirisha baadhi ya miili ya walouliowa karibu na Mandera yawasili kwnye uwanja wa ndege wa Wilson, Nairobi, Dec. 2, 2014.

Rais Uhuru Kenyatta, amepokea ripoti kutoka kamati ya bunge, yenye lengo la kuondowa vizuizi vya kisheria na utawala vinavyozuia serikali kupambana vilivyo na makundi yenye silaha, kama vile al Shabab ya Somalia, amesema msemaji wa rais.

Akizungumza na Sauti ya Amerika siku ya Alhamisi Manoah Esipisu, amesema Rais Kenyatta aliiomba kamati ya Ulinzi na Usalama ya bunge mapema wiki hii kutafakari juu ya mkakati wa usalama na kutoa mapendekezo ya namna ya kuondowa vizuizi vya kisheria vinavyozuia vita kamili dhidi ya ugaidi.

Your browser doesn’t support HTML5

Abdushakur azungumza na Esipisu juu ya usalama.

Esipisu anasema "kazi ya usalama ni jukumu la serikali kuu ya taifa, na serikali ya taifa inafanya juu chini kuhakikisha kwamba usalama umeimarishwa. Jambo tunalotilia maanani na umuhimu ni kwamba serikali inataka kuhakikisha vikosi vya polisi vina vifaa vinavyo hitajiki kupambana na magaidi."

Hata hivyo, msemaji wa rais amepinga hoja kwamba serikali haina mkakati thabiti wa kupambana na magaidi na hakuna haja ya kuwepo na mjadala wa kitaifa juu ya usalama, kama vile wananchi wengi wanavyopendekeza.