Michel Kafando ameapishwa kuwa Rais wa mpito wa Burkina Faso, akiwa na wajibu wa kuipeleka nchi hiyo ya afrika magharibi katika utawala wa kiraia.
Rais Kafando ameapa kuheshimu katiba na makubaliano ya mpito katika sherehe mjini Ouagadougou, iliyoonyeshwa moja kwa moja na televisheni Jumanne.
Rais huyo mpya anawajibu wa kumtangaza waziri mkuu na kusaidia kuundwa kwa serikali ya mpito yenye watu 25 kuongoza Burkina Faso mpaka uchaguzi mpya mwakani.
Rais Kafando alichaguliwa kuwa kiongozi wa mpito Jumatatu na kamati iliyokuwa na wawakilishi wa kijeshi, wanasiasa, viongozi wa taasisi za kiraia na kidini.
Akiwa na umri wa miaka 72 Rais Kafando haruhusiwi kugombea tena urais katika uchaguzi wa mwakani.