WHO yasema chanjo ya Ebola kuanza kutumika January.

Mkurugenzi wa WHO Margaret Chan AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI.

Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani - WHO - Dr. Marie Paule Kieny alisema Jumanne majaribio ya dawa ya chanjo ya Ebola yanaendelea huko Ulaya Marekani na Afrika, na kwamba kama chanjo hizo zikionekana kuwa salama kunaweza kuwa na majaribio Afrika magharibi mwezi Januari , wakitumia maelfu kwa maelfu ya dozi.

Akiongea na waandishi huko Geneva Dr. Kieny hakusema ni lini chanjo ya Ebola inaweza kupatikana duniani kote.

Hakuna dawa wala chanjo ya ugonjwa huo ambao umeuwa zaidi ya watu 4,500 huko Afrika Magharibi mwaka huu.

Jumatatu WHO ilitangaza taifa la Nigeria kuwa halina tena ugonjwa wa Ebola baada ya siku 42 kupita bila ripoti za kesi mpya a ugonjwa huo.